Pata taarifa kuu
LUANDA-ANGOLA

Mgogoro wa kisiasa nchini Malawi, Zimbabwe na Madagascar kutawala mazungumzo ya mkutano wa viongozi wa SADC

Nembo ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC
Nembo ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC SADC site

Wakati viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC wakitarajiwa kuanza mkutano wao mjini Luanda Angola siku ya jumatano, ajenda kubwa inayotarajiwa kujadiliwa ni migogoro ya kisiasa katika nchi za Malawi, Zimbabwe na Madagascar.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wa nchi 15 wanatarajiwa kiujadili migogoro ya kisiasa katika mataifa hayo huku wachambuzi wa mambo wakisema kuwa wanatarajia kuona nchi wanachama wakitekeleza kwa vitendo maazimio yao kuliko kuzungumza.

Mkutano huo unaanza huku viongozi hao wakikosolewa kwa kushindwa kutekeleza maazimio kadhaa waliyokubalina katika mkutano uliopita ikiwemo suala la rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kushindwa kutekeleza maazimio yaliyofikiwa kati yake na waziri mkuu Morgan Tsvangirai ya kugawana madaraka na kuanza mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.

Mbali na nchi ya Zimbabwe kujadiliwa, mkutano huo pia unatarajiwa kuzungumzia hali ya kisiasa nchini Madagascar ambapo viongozi hao waliinyang'anya uanachama nchi hiyo mwaka 2009 baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomweka madarakani rais Andy Rajoelina.

Viongozi hao pia wanakabiliwa na changamoto ya kumshawishi kiongozi aliyepinduliwa madarakani Mark ravalomanana kukubali kutia saini makubalino ya Jumuiya hiyo ya kutaka kufanyika kwa mazungumzo kati yake na Rajoelina ili kumaliza mzozo wa kisiasa ulipo kati yao.

Nchi za Malawi na Swaziland pia zinatarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo ambapo majuma kadhaa yaliyopita serikali ya rais Bingu wa Mutharika wa Malawi ilijikuta ikikabiliwa na maandamano makubwa yaliyosababisha vifo vya watu 19 huku Swaziland ikikumbwa na mtikisiko wa kifedha.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.