Pata taarifa kuu
Malawi

Rais wa Malawi awaonya wapinzani kuhusu maandamano

RFI

Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika ametangaza vita dhidi ya wapinzani wake wanaopanga kufanya mkesha wa kitaifa tarehe 21 mwezi ujao kupinga sera za Serikali yake.

Matangazo ya kibiashara

 

Katika hotuba yake, Mutharika amesema Serikali yake ina nguvu ya kuwakamata waratibu wa maandamano ikiwa yatafanyika siku hiyo na kuapa kuwatia nguvuni ikiwa watakaidi agizo hilo.
Wakosoaji wanamshutumu Mutharika kwa kuwa dikteta na kuwa hafanyii kazi matatizo ya kiuchumi yanayoikumba nchi hiyo hali inayosababisha wafadhili wao wa kigeni kusitisha misaada nchini humo.
Mwezi uliopita watu 19 waliuawa baada ya vikosi vya usalama nchini humo kuwafyatulia risasi waandamanaji.
Awali, Asasi za kiraia nchini humo ziliitisha mkesha wa nchi nzima tarehe 17 mwezi huu kupinga utawala wa Mutharika kuomba kutofanyika kwa mkesha huo kwa kuhofia usalama wa raia na mali zao.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.