Pata taarifa kuu
TANZANIA-MALAWI

Mawaziri wa Mambo ya nje wa Tanzania, Malawa wakutana kuzungumzia mvutano wa umiliki wa Ziwa Nyasa

RFI

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Malawi na Tanzania hii leo wanatarajiwa kukutana kwenye mji wa Mzuzu kaskazini mwa nchi ya Malawi kuzungumzia mgogoro wa kimipaka ulioibuka hivi karibuni kuhusu ziwa Nyasa.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unafanyika baada ya rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na rais wa Malawi Joyce Banda kukutana nje ya mkutano wa SADC mjini Maputo msumbiji na kukubaliana kuendelea na mazungumzo zaidi kuhusu mpaka wa ziwa Nyasa.

Katika mazungumzo yao rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na rais wa Malawi Joyce Banda walikubaliana kuunda kamati itakayoshughulikia mvutano huo ili kuumaliza kwa njia za kidiplomasia.

Mvutano wa ziwa Nyasa umezuka baada ya nchi ya Malawi kutoa leseni ya utafutaji mafuta na gesi kwenye ziwa hilo kwa kampuni moja ya Uingereza jambo ambalo serikali ya Tanzania imesema kampuni hizo zimeingia hadi upande wa Tanzania jambo ambalo halikubaliki.

Awali Serikali ya Tanzania iliapa kulinda mipaka yake kwa gharama yoyote na hata kuwa tayari kuingia vitani na Malawi endapo italazimika kufanya hivyo na kuyaonya makampuni yaliyokuwa yakifanya utafiti huo kuacha mara moja kufanya hivyo.

Serikali ya Malawi kupitia kwa Rais Banda imesema kuwa haitakuwa tayari kupigana vita na ndugu zao wa Tanzania na hata kama njia za kidiplomasia zitashindikana bado kutakuwa na njia nyingine za kushughulikia tatizo hilo lakini si vita.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.