Pata taarifa kuu
Nigeria

Mama wa Waziri wa fedha wa Nigeria Ngozi Okonjo-Iweala atekwa nyara

Mama wa Waziri wa fedha wa Nigeria na Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Benki ya Dunia Ngozi Okonjo-Iweala alitekwa nyara akiwa nyumbani kwake Kusini mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Serikali katika jimbo la Delta imethibitisha utekwaji nyara huo wa Profesa Kamene Okonjo na watu wasiojulikana katika kijiji chake cha Ogwashi Uku.

Polisi wanasema kwa sasa ni  vigumu kubaini ni akina nani waliomteka nyara mama huyo, licha ya Waziri huyo wa fedha kupokea vitisho vya mara kwa mara.

Okonjo Iweala amekuwa akisifiwa mno na wananchi nchini humo kwa kuhakikisha kuwa anasadia kumaliza visa vya ufisaidi nchini humo.

Waziri huyo wa fedha, mapema mwaka huu alikuwa anawania wadhifa wa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Dunia.

Kundi la kigaidi la  Boko Haram limekuwa likikashifiwa kusababisha ukosefu wa usalama Kaskazini mwa nchi hiyo na kusababisha mauaji ya  mamia ya watu .

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.