Pata taarifa kuu
MISRI

Morsi kufikishwa kizimbani tarehe 4 mwezi Novemba

Mahakama nchini Misri imetenga tarehe 4 mwezi wa Novemba kuanza kusikilizwa kwa kesi ya uchochezi na mauaji inayomkabili rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi.

Matangazo ya kibiashara

Morsi atafika kizimbani akiandamana na washtakiwa wengine 14 wanaotuhumiwa kuchochea mauaji hayo wakati wa maandamani mwezi Desemba mwaka uliopita, miezi saba kabla ya  uongozi wake haujapinduliwa na jeshi.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa kushtakiwa kwa Morsi huenda kukasababisha maandamano zaidi nchini humo kipindi hiki hali ya wasiwasi ikiendelea kutanda baada ya watu 57 kuuliwa Jumapili iliyopita wakati wa makabiliano na polisi jijini Cairo.

Upande wa Mashtaka unamtuhumu Morsi kuchochea maaandamano na mauji ya raia wasiokuwa na hatia mwaka uliopita kwa kutumia mamlaka yake vibaya kama kiongozi wa taifa hilo.

Wapinzani wa Morsi walianza kupiga kambi nje ya Ikulu jijini Cairo kumtuhumu kushindwa kutekeleza mabadiliko muhimu aliyowaahidi alipoingia madarakani baada ya mapinduzi dhidi ya rais wa zamani Hosni Mubarak.

Miongoni mwa ahadi hizo ni pamoja na  usawa wa kila raia nchini humo,  kuimarisha sekta ya uchumi na kuunda nafasi za kazi hasa kwa vijana.

Jumuiya ya Kimataifa ikiongozwa na Umoja wa Ulaya imekuwa ikitaka wanasiasa nchini humokuzungumza na upinzani ili kuleta suluhu ya kisiasa nchini humo .

Mkuu wa sera za nje wa Umoja huo Catherine Ashton amekuwa katika mstari wa mbele kuwashawishi viongozi wa serikali ya mpito kumwachilia huru Morsi kama ishara ya kuleta upatanishi kati ya wafuasi na wapinzani wake.

Wafusi wa Morsi wamekuwa wakiandamana mara kwa mara kushinikiza kurudishwa madarakani kwa kiongozi wao wanaosema alichaguliwa kidemokrasia.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.