Pata taarifa kuu
MISRI

Wamisri wafanya kumbukumbu ya mapinduzi ya kijeshi yaliyoangusha utawala wa Hosni Mubarak

Mamia ya Wamisri wamekusanyika katika eneo la Tahrir jijini Cairo jana Jumatatu kuadhimisha kumbukumbu ya maandamano dhidi ya jeshi mwaka 2011, maandamano ambayo yalichochea mapigano makali baina ya waandamanaji na vikosi vya usalama. Maandamano hayo yanakuja miezi minne baada ya jeshi kwa mara nyingine kuchukua madaraka baada ya kumwondoa madarakani aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Mohamed Morsi, kufuatia maandamano makubwa dhidi ya utawala wake wa misukosuko uliodumu kwa mwaka mmoja.

Matangazo ya kibiashara

Maandamano ya mwaka 2011 katikati mwa Cairo yalikuwa dhidi ya Baraza Kuu la Vikosi vya Jeshi, serikali hiyo ya kijeshi ambayo ilichukua madaraka baada ya kuipindua serikali ya kidikteta ya Hosni Mubarak mwaka 2011.

Takribani watu 43 waliuawa na wengine zaidi ya 3,000 kujeruhiwa katika makabiliano baina ya waandamanaji na Maafisa Usalama Novemba 19 mwaka 2011, ikiwa ni miezi minne pekee baada ya miezi 9 ya kuondoka madarakani kwa Hosni Mubarak.

Serikali ya mpito hiyo jana ilizindua kumbukumbu maalumu kama ishara ya kuwakumbuka waliopoteza maisha katika mapinduzi ya mwaka 2011, hata hivyo wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu wamekosoa utawala huo wakisema hakuna mabadiliko yoyote chanya yaliyoshuhudiwa tangu mapinduzi hayo.

Bado hali ya usalama imeendelea kuwa tete nchini humo hasa baada ya kuondolewa madarakani kwa Morsi ambaye wafuasi wake wameendelea kuandamana na kukabiliana na vikosi vya usalama wakishinikiza kiongozi wao arejeshwe madarakani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.