Pata taarifa kuu
KENYA

Watatu wajeruhiwa katika shambulizi la guruneti mjini Garissa Kenya

wataalamu wa vilipuzi wakifanya uchunguzi  baada ya sahmbulio la bomu tarehe 23 Mei 2014 mjini Mombasa mtaa wa Biashara
wataalamu wa vilipuzi wakifanya uchunguzi baada ya sahmbulio la bomu tarehe 23 Mei 2014 mjini Mombasa mtaa wa Biashara REUTERS/Joseph Okanga

Watu watatu wamejeruhiwa katika shambulizi la guruneti katika mji wa Garisa nchini Kenya jana Jumamosi mkuu wa polisi wa eneo hilo amethibitisha. 

Matangazo ya kibiashara

Kati ya vijana wawili au watatu wanadaiwa kurusha guruneti hilo ndani ya karakana na kujeruhi mafundi makenika watatu, kabla yakukimbia ameeleza mkuu wa polisi katika kaunti ya Garissa Charles Kinyua.

Hata hivyo sababu za kufanya shambulio katika eneo hilo jirani na mpaka wa Somalia hazikujulikana.

Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya maguruneti na bunduki ambayo mara kwa mara yanadaiwa kutekelezwa na waasi wa kiislam wa kundi la Al Shabab na mara kwa mara yamekuwa yakilemga idara za usalama kama polisi , tangu nchi hiyo ipeleke wanajeshi wake nchini Somalia kupambana na Al Shabab chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika kinacholinda amani nchini Somalia AMISOM
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.