Pata taarifa kuu
MISRI-Kiapo

Abdul Fattah al-Sisi kuapa kuiongoza Misri leo

Aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Misri, Abdel Fatah al-Sisi kula kiapo cha kuiongoza Misri
Aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Misri, Abdel Fatah al-Sisi kula kiapo cha kuiongoza Misri Reuters

Mkuu wa Zamani wa majeshi Abdel Fattah al-Sisi anaapishwa hii leo kuwa rais mpya wa taifa la Misri baada ya miaka mitatu ya mgogoro wa kisiasa tangu kuondolewa madarakani kwa rais wa muda mrefu Hosni Mubarak.

Matangazo ya kibiashara

Majeshi ya usalama yamesambazwa katika maeneo muhimu kuzunguka mji mkuu Cairo katika maandalizi ya siku hii muhimu itakayofanyikia katika mahakama ya juu ya kikatiba.

Mkuu huyo wa majeshi aliyestaafu cheo hicho siku chache zilizopita aliongoza harakati za kumpindua raisi aliyekuwepo madarakani mohamed Morsi.

Hata hivyo anaingia madarakani akiwa na uhasama kati yake na wafuasi wa chama cha Mohamed Morsi,Muslim Brotherhood ambao wakati wa uchaguzi walitaka raia kutopiga kura.
 

Ni sherehe za aina yake nchini humo kwa vile kiongozi huyo anaonekana kupendwa na raia wengi ambao wanamatumaini ya uongozi wa Al Sisi kuleta mabadiliko nchini humo.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.