Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA-AL-MOURABITOUNE-Usalama

Mali : Al-Mourabitoune yakiri kumua mwanajeshi wa Ufaransa

Kambi ya wanajeshi wa Ufaransa katika eneo la Gao nchini Mali.
Kambi ya wanajeshi wa Ufaransa katika eneo la Gao nchini Mali. Olivier Fourt/RFI

Kundi la kislamu la Al-Mourabitoune linaloendesha harakati zake nchini Algeria la Mokhtar Belmokhtar, limekiri kupitia shirika la habari la kibinafsi la Mauritania Alakhbar kwamba limehusikana shambulio la kujitoa muhanga la Julai 14 ililomuua mwanajeshi wa Ufaransa kaskazini mwa Mali.

Matangazo ya kibiashara

“Mwanamgambo wetu alifaulu kulipua gari lake lililokua limebeba vilipuzi dhidi ya kikosi cha jeshi kiliyovamia eneo la Al-Moustarat, na kumuua mwanajeshi mmoja wa Ufaransa na kuwajeruhi wengine wengi katika eneo la Gao (kaskazini mwa Mali)”, msemaji wa Al-Mourabitoune, Abou Aassim El-Mouhajir, amelithibitishia shirika hilo.

“Shambulio hilo lilikua ni jibu kwa Ufaransa ambayo hivi karibuni ilidai kwamba operesheni ya wanasheshi wake Serval, ilfaulu kuvunja makundi ya kislamu yenye silaha, amesema El-Mouhajir.

Operesheni hio Servali iliyoanzishwa Januari mwaka 2013 ili kuyatokomeza makundi ya kislamu yenye mafungamano na kundi la Al Qaeda, ambayo yalikua yakishikilia kwa muda wa miezi tisa kaskazini ya Mali, ilimalizika hivi karibuni, na nafasi yake ikachukuliwa na operesheni iitwayo Barkhane ambayo itapambana na ugaidi katika mataifa mengi yaliyo katika ukanda wa Sahel na kusini mwa jangwa la Sahara.

“Operesheni Serval ambayo ilianzishwa dhidi ya jamii ya waislamu imeingiza eneo hili katika vita vya kiraia na machafuko ya kikabila, wakati utawala wa kislamu ulikua umekomesha mashafuko hayo”, ameongeza El-Mouhajir.

Msafara wa magari ya wanajeshi wa Ufaransa katika kijiji cha Bemba, kiliopo kati ya Tombouctou na Gao kaskazini mwa Mali.
Msafara wa magari ya wanajeshi wa Ufaransa katika kijiji cha Bemba, kiliopo kati ya Tombouctou na Gao kaskazini mwa Mali. AFP PHOTO/PHILIPPE DESMAZES

Hayo yanajiri wakati waziri wa ulinzi wa Ufaransa akiwa ziarani nchini Mali, na atajielekeza hadi katika eneo la Gao alikouawa mwanajeshi huyo wa Ufaransa, Julai 14, siku ambayo Ufaransa ilikua ikisheherekea maadhimisho ya miaka 100 tangu kumalizika kwa vita vya kwanza.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.