Pata taarifa kuu
MALI-MINUSMA-AZAWAD-GATIA-Uasi-Usalama

Mali: mazungumzo ya amani yaahirishwa

jeshi la Mali likipiga doria katika jimbo la Gao.
jeshi la Mali likipiga doria katika jimbo la Gao. Olivier Fourt/RFI

Mkuu wa tume ya umoja wa Mataifa nchini Mali Minusma, Hervé Ladsous, ameyataka makundi yenye silaha kutoa ushiriki wao ili kupiga vita ugaidi.

Matangazo ya kibiashara

Wawakilishi wa makundi hayo wamebaini kwamba tangazo hilo la mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali halieleweki.

Wakati huo huo, mkutano wa uzinduzi wa mazungumzo ya amani nchini Mali umeahirishwa.

Kila mmoja ana maelezo yake lakini makundi yote yako tayari kwa mazungumzo. Hata hivo wawakilishi wa makundi hayo wamekataa kunyooshewa kidole kwamba makundi yenye silaha yanahusika katika mashambulizi ya kigaidi.

Wawakiliahi wa makundi hayo wamebaini kwamba hata makundi hayo ymekua yakilengwa na mashambulizi ya kigaidi, huku wakisema kwamba hawana uwezo wa kuendesha vita dhidi ya makundi ya wapiganaji wa kiislam.

Kwa upande wa makundi yanayoshirikiana kwa karibu na utawala wa Bamako, hususan Gatia, wameyatuhumu makundi yanayoendesha harakazi zao katika jimbo la Kidal kwamba hayatowi ushiriki wao kwa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma). Lakini wamebaini kwamba hakuna operesheni yoyote kati ya Minusma na makundi yenye silaha ambayo itafanyika bila kuwepo na mkataba waliotiliana saini.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.