Pata taarifa kuu
Misri

Mubarak afutiwa mashitaka ya mauaji dhidi ya waandamanaji nchini Misri

Mwanamke  akifurahia uamuzi wa mahakama dhidi ya rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak
Mwanamke akifurahia uamuzi wa mahakama dhidi ya rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak REUTERS/Asmaa Waguih

Mahakama kuu nchini Misri jana Jumamosi imemwondolea mashitaka ya mauaji rais wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak kutokana na vifo vya waandamanaji wakati wa vuguvugu la mapinduzi ya mwaka 2011 baada ya kujaribu kutaka kusalia tena madarakani huku akiwa ameongoza nchi hiyo kwa miaka 30. 

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umechochea hasira ya wapinzani wa Mubarak ambapo karibu watu 1000 walikutana katikati mwa jiji la Cairo kupinga serikali.

Wizara ya afya imesema kuwa mtu mmoja amepigwa risasi na kufariki dunia wakati Polisi wa kutuliza ghasia nchini Misri wakijaribu kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakiandamana kupinga uamuzi ya mahakama nchini humo.

Aidha mahakama imemwondolea rais huyo wa zamani mashataka ya rushwa, lakini ataendelea kubaki kizuizini kwa sababu anatumikia kifungo cha miaka mitatu katika kesi nyingine ya rushwa.

Maaafisa wengine saba waliohudumu kwenye serikali ya Mubarak akiwemo waziri wa zamani wa mambo ya ndani anayeogopwa Habib al Adly pia wamefutiwa mashitaka ya mauaji ya watu 800 waliouawa katika mapinduzi hayo.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.