Pata taarifa kuu
MALI-NIGER-MUJAO-USALAMA

Watu watatu watekwa nyara Mali

Wapiganaji wa kundi la Mujao katika mji wa Gao, Julai 16 mwaka 2012.
Wapiganaji wa kundi la Mujao katika mji wa Gao, Julai 16 mwaka 2012. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Baada ya jeshi la Niger kushambuliwa hivi karibuni na kundi la wapiganaji wa kiislam la Mujao, kundi hilo limewateka nyara watu watatu nchini Mali karibu na mpaka wa Niger.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilitokea Jumatano jioni katika ardhi ya Mali, lakini karibu na kijiji cha Bani Bangou nchini Nigeria, ambacho kilishambuliwa hivi karibuni na wapiganaji wa kundi la Mujao.

Watu wanne walikua ndani ya gari wakati watu sita wenye silaha wakiwa kwenye pikipiki walipowashambulia. Watu hao wenye silaha walifyatua risasi hewani. Watu watatu waliokua ndani ya gari hiyo walikamatwa na baadae walifungwa pingu mikononi. Watu hao wenye silaha walimlazimisha dereva kuwapa funguo za gari.

Watu hao ni wapiganaji wa kundi la Mujao, lenye mafungamano na kundi la Dola la Kiislam. Inaonekana kuwa wapiganaji hao walikua wakiwatafuta watu hao waliotekwa nyara, ambao wote ni kutoa Mali. Baada ya tukio hilo, mateka na baadhi ya watekaji nyara walielekea kaskazini mashariki mwa Mali na watekaji nyara wengine walijielekeza, kwenye pikipiki, kuni mwa Mali.

Kundi la Mujao limekua likiendesha harakati zake kwenye mpaka wa Mali na Niger.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.