Pata taarifa kuu
SENEGAL-AFRIKA-MKUTANO-USALAMA-AMANI-

Mkutano kuhusu amani na usalama Dakar

Askari wa ufaransa katika operesheni Barkhan nchini Mali, Novemba 5 mwaka 2014.
Askari wa ufaransa katika operesheni Barkhan nchini Mali, Novemba 5 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney

Marais, viongozi wa serikali na Mawaziri wa ulinzi wanatazamiwa kushiriki kwa muda wa siku mbili mkutano kuhusu amani na usalama barani Afrika, mkutano ambao unafanyika katika mji mkuu wa senegal Dakar.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa viongozi waotazamiwa kushiriki mkutano huo ni pamoja na rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta, rais wa Chad Idriss Déby, rais wa Mauritania Ould Abdellaziz, pamoja na mwenyeji wa mkutano huo rais wa Senegal Macky Sall.

Mkutano huo ambao unaanza leo Jumatatu Desemba 15, unatazamiwa kumalizika Jumanne Desemba 16 jioni. Lengo la mkutano huo ni kuboresha ushirikiano katika sekta ya usalama na amani.

Watafiti na wawakilishi wa mashirika mbalimbali watahuduria mkutano huo ambao wengi wanadhani kwamba utaleta changamoto katika sekta hususan ya usalama barani Afrika. Serikali ya Senegal imebaini kwamba mkutano huo ni muhimu kwa usalama na amani barani Afrika, hususan katika mataifa yanayokabiliwa na mdororo wa usalama kutokana na machfuko ya wenyewe kwa wenyewe, aidha machafuko yenye misingi ya kisiasa na kidini.

Hata hivyo Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, tangu mwanzoni mwa mwaka 2014, amekua akiyatembelea mataifa ya Afrika kwa lengo la kudumisha usalama na amani. Ufaransa imekua ikichangia kwa kuleta amani katika mataifa ya Afrika, hususan mataifa ya Afrika Magharibi.

Ufaransa inaweza ikasaidia kusuluhisha katika mzozo unaoendelea kushuhudiwa nchini Nigeria, wakati ambapo kundi la Boko Haram linaendelea na mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Lakini sasa kinachoshuhudiwa katika mkutano huo unaofanyika chini Senegal ni kwamba mataifa mengi yanayozungumza Kingereza yalisusia mkutano huo, na inaonekana kuwa mataifa karibu yote yanayozungumza Kifaransa yamewakilishwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.