Pata taarifa kuu
RWANDA-MALI-MINUSMA-ICTR-Uhalifu

Aibu kwa UN baada ya kuondoka Kazura

Jeneral Jean Bosco Kazura. Aliye kuwa mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani Mali.
Jeneral Jean Bosco Kazura. Aliye kuwa mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani Mali. David Baché / RFI

Mkataba wa afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Rwanda, Jean Bosco Kazura, ambaye aliongoza askari wa kikosi cha umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma), kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu, haujaongezwa.

Matangazo ya kibiashara

Kazi yake ilikuwa bado ikipongezwa wiki hii kwenye RFI, na Hervé Ladsous, mkuu wa oparesheni za kulinda amani.

Desemba mwaka 2013, mwandishi wa habari wa Canada, Judi Rever, alimtuhumu afisa huyo wa ngazi ya juu katika jeshi la Rwanda kuhusika na makosa ya uhalifu wa kivita katika mwaka 1994, wakati alikua afisa wa ngazi ya juu katika kundi la waasi wa zamani wa (RPF) liliyokua likiongozwa na rais Paul Kagame.

Mpaka sasa, Umoja wa Mataifa ulikua umesalia kimya kuhusu madai hayo lakini tangu kuondoka kwa jenerali Kazura, kauli mbalimbali ziemeanza kusikika. Idara ya Oparesheni ya kulinda amani imesema imekua ikijadiliana kuhusu suala hilo.

" Kuondoka kwa jenerali Kazura hakuhusiani na madai ya mwandishi wa habari wa Canada," imebaini Idara ya Oparesheni ya kulinda amani, huku Idara hiyo ikisikitishwa kuona mkataba wa mkuu wa kikosi cha Minusma haujaongezwa.

Hata hivyo, ili kuthibitisha tuhuma zilizomo katika makala ya Judi Rever, New York imesema rasmi kwamba ilikutana Jumatano Desemba 17 na Shirika la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu na Mahakama ya kimataifa ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR). Hakuna taasisi moja kati ya hizo iliyopinga uteuzi au kuendelea kuongoza kwa jenerali Kazura kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma).

Hata hivyo, Shirika la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu limesema kwamba halikua na uwezo - juu ya msingi wa nyaraka zake, kuthibitisha madai ya mwandishi wa habari wa Canada. Itakumbukwa kwamba Judi Rever wala mashahidi wake hawakuwahi kuitishwa na Umoja wa Mataifa ili wasikilizwe.

Shirika la Umoja wa mataifa la haki za binadamu lilianzishwa mwaka 1993 na lilikuwa bado changa mwaka 1994. Mwandishi wa habari wa Canada alikuwa alipendekeza katika Idara ya Oparesheni ya kulinda amani kushauriana na ICTR.

Mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa ilikua na majukumu ya kushughulikia makosa ya uhalifu wa mauaji ya kimbari lakini pia uhalifu wa kivita uliofanywa mwaka1994, pamoja na yale yaliyotekelezwa na kundi la waasi wa zamani la RPF lililokua likiongozwa na rais wa Rwanda Paul Kagame.

Hayo yakijiri, ICTR iko mbioni kufunga milango yake mwaka huu bila hata hivyo kuheshimu sehemu ya pili ya majukumu yake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.