Pata taarifa kuu
Soka Barani Afrika-AFCON 2015

Moussa Sow aiokoa Senegal

Moussa Sow kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Senegal, aiokoa timu yake kwa kuifungia bao la ushindi katika michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Ghana..
Moussa Sow kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Senegal, aiokoa timu yake kwa kuifungia bao la ushindi katika michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Ghana.. REUTERS/Murad Sezer

Michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika imeendelea leo Jumatatu Januari 19 nchini Equatorial Guinea kwa siku yake ya tatu, ambapo Senegal na Ghana walifungua dimba katika mechi ya kwanza.

Matangazo ya kibiashara

Mechi kati ya timu hizo mbili imekua ni yenye kuvutia, licha ya kuwa Ghana imesalimu amri kwa kukubali kufungwa mabao 2-1. Ghana ilianza kuliona lango la Senegal katika kipidi cha kwanza.

Bao la Ghana limewekwa kimyani na Andrés Ayew katika dakika ya 14 ya mchezo kwa mkwaju wa penalti. Hadi dakika 45 za mchezo katika kipindi cha kwanza, Ghana imekua ikiongoza kwa bao 1 kwa 0 dhdi ya Senegal.

Baada ya mapumziko, Senegal ilikuja juu, huku Ghana ikionekana kupoteza muelekeo, na nguvu ilizokua imeanza nazo.

Katika dakika ya 58 mchezaji wa klabu ya Stoke ya Uingereza, Mame Birame Diouf, aliliona lango la Ghana na kuandikisha bao la kusawazisha. Ghana iliendelea kutawala mpira, hadi katika dakika ya 90 ya mchezo, timu hizo mbili zilikua sare ya bao 1-1.

katika dakika ya tatu ya nyongeza, Moussa Sow alikuja juu na kupachika bao la pili na la ushindi kwa timu yake ya taifa. Moussa Sow anaichezea klabu ya Uturuki ya Fenerbahçe

Senegal na Ghana ni miongoni mwa timu inne za kundi C.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.