Pata taarifa kuu
MISRI-MAUAJi-HAKI-SHERIA

Misri: Miaka miwili ya ukandamizaji

Abdel Fattah Al-Sissi, rais wa Misri.
Abdel Fattah Al-Sissi, rais wa Misri. REUTERS/The Egyptian Presidency/Handout

Nchini Misri, Julai 3 ni siku ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka miwili ya kuangushwa kwa utawala wa Mohamed Morsi, rais wa kwanza aliye chaguliwa katika misingi ya kidemokrasia katika zama za baada ya Mubarak, na kuingia madarakani kwa mtu aliye kuwa kiongozi wa majeshi ya Misri: Abdel Fatah al -Sissi.

Matangazo ya kibiashara

Miaka hii miwili imekua ni ya mapambano dhidi ya wapiganaji wa kijihadi katika eneo la Sinai, lakini pia ukandamizaji na mauaji dhidi ya wafuasi wa Muslim Brotherhood na wale wa vyama vya upinzani.

Takwimu zinaonesha jinsi gani utawala wa Abdel Fatah al-Sisi ulivyokua ukiwakandamiza wapinzani wake. Zaidi ya waandamanaji 1,400 wanaomuunga mkono Morsi waliuawa katika majira ya joto mwaka 2013 na zaidi ya 15,000 wengine walifungwa. Mamia kati yao walihukumiwa adhabu ya kifo katika kesi za ajabu, kesi ambazo hazikufuatisha sheria, kwa mujibu wa mashirika yanayotetea haki za binadamu.

Miaka miwili baada ya kuingia madarakani, Abdel Fatah al-Sisi hakukandamiza wafuasi wa Muslim Brotherhood peke yao, aliwakandamiza pia viongozi na wanaharakati waliopambana dhidi ya tawala za kimla katika enzi hizo za kiarabu, wakiwemo vijana waliosimama kidete na kuandamana mwezi Januari mwaka 2011 dhidi ya Hosni Mubarak.

Hata hivyo pamoja na tathmini hii katika masuala ya haki za binadamu iliyokosolewa kwa kiasi kikubwa, rais wa Misri ameendelea kuungwa mkono na kuheshimiwa na baadhi ya nchi za magharibi. Mataifa haya yanabaini kwamba utawala mpya wa Misri umekua ukipambana vilivyo ili taifa hilo liwe lenye utulivu na amani.

"Utawala umejiwekea wenyewe tishio linaloukabili leo"

Raia wengi wa Misri wanaendeleakumuunga mkono rais Sissi. Pamoja na kuongezeka kwa mapigano katika eneo la Sinai na kuongezeka kwa makundi ya kijihadi, wakazi wengi wa Misri, waliokandamizwa na utawala wa Muslim Brotherhood, wameendelea pia kumchukulia Abdel Fatah al-Sisi kama rais anayefaa kwa kuimarisha utulivu na usalama kwa nchi yao.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.