Pata taarifa kuu
TANZANIA-SIASA

CCM yamsaka mtu atakaepeperusha bendera yake katika uchaguzi ujao

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, anaye maliza muda wake wa kuliongoza taifa la Tanzania, wakati chama cha CCM kikimsaka mtu atakayepeperusha bendera yake katika Uchaguzi mkuu ujao.
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, anaye maliza muda wake wa kuliongoza taifa la Tanzania, wakati chama cha CCM kikimsaka mtu atakayepeperusha bendera yake katika Uchaguzi mkuu ujao. TZ govt

Nchini Tanzania, wafuasi wa chama tawala CCM wanasubiri kufahamu ni nani atakayepeperusha bedera ya chama hicho wakati wa uchaguzi wa urais Mwezi Oktoba.

Matangazo ya kibiashara

Watu 38 waliomba kupepersha bendera ya chama hicho na mchakato wa kumpata mgombea ulianza Jumatano wiki hii baada ya kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama.

Leo Alhamisi Kamati kuu ya chama itakutana kwa lengo la kutazama jinsi ya kupinguza majina ya wagombea hadi kufikia majina matano tu.Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ina wanachama takribani 32.

Halmashauri kuu ya chama inatazamiwa kukutana Ijumaa Julai 10 ambapo itachuja majina hayo matano hadi kufikia matatu kupitia mtindo wa kupiga kura. Majina haya matatu ndiyo yatakayokwenda katika Mkutano Mkuu wa Chama ambao ndio utakaochagua jina moja la mgombea urais kwa tiketi ya chama tawala cha CCM

Mkutano mkuu wa chama cha CCM unajumisha wanachama 2100 ikiwa ni pamoja na Wabunge wa CCM Tanzania bara na wawakilishi wengine kutoka Zanzibar lakini pia wawakilishi wa chama kutoka ngazi mbalimbali hadi ngazi za chini.

Hata hivyo mkutano huu mkuu wa chama cha CCM umepangwa kufanyika tarehe 11 hadi 12 Julai mwka 2015.

Idadi ya wanachama waliojitokeza kuchukua fomu na kutafuta ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea urais wa chama hicho ilifikia 42, ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya CCM na nchi kwa ujumla.

Baadhi ya wanoatafuta kuteuliwa kuwa wagombea wa chama hicho wamehusishwa na kashfa kadhaa za matumizi mabaya ya madaraka na rushwa vilivyoisababishia serikali hasara kubwa na kuzua mjadala mzito miongoni mwa Watanzania.

Hayo yakijiri rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Alhamisi anatarajiwa kulivunja bunge la taifa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

Bunge nchini humo litakumbukwa kujadili na kupitisha rasimu ya Katiba mpya katika uongozi wa rais Kikwete.

Hata hivyo wabunge wa upinzani ambao walisusia ufunguzi wa bunge hilo wakati rais Kikwete alipochaguliwa tena kwa muhula wa pili mwaka 2010, wamesema watasusia tena hivi leo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.