Pata taarifa kuu
URUSI-MISRI-AJALI YA NDEGE

Marekani: "hakuna dalili ya kitendo cha kigaidi kwa sasa"

Picha ya zamani ya James Clapper (kulia), Mkuu wa Idara ya Upelelezi wa Taifa nchini Marekani (DNI), akitoa ushahidi pamoja John Brennan (kushoto).
Picha ya zamani ya James Clapper (kulia), Mkuu wa Idara ya Upelelezi wa Taifa nchini Marekani (DNI), akitoa ushahidi pamoja John Brennan (kushoto). AFP/AFP

Mkuu wa Idara ya Ujasusi nchini Marekani James Clapper amebaini Jumatatu wiki hii mjini Washington kwamba hakuna dalili zozote kwa sasa kuwa kitendo cha kigaidi kilikua chanzo cha ajali ya ndege ya Urusi iliyotokea katika jangwa la Sinai, nchini Msri.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Idara ya Ujasusi (DNI) James Clapper amebaini pia kwamba kundi la Islamic State halina uwezo wa kudungua ndege ya biashara ikiwa angani, huku akiongeza kuwa hawezi kupinga moja kwa moja hoja hiyo.

Ndege hiyo yenye chapa A321-200 ya shirika la ndege la Urusi la Metrojet ilianguka Jumamosi Alfajiri katika jangwa la Sinai, baada ya kupaa kutoka mji wa mapumziko wa Misri wa Sharm el-Sheikh ikiwa njiani kuelekea St Petersburg.

" EI ilikiri kuhusika na udunguaji wa ndege hiyo ", ameendelea Bwa. Clapper, akimaanisha uthibitisho uliotolewa na tawi la kundi la Islamic State nchini Misri ambalo lilibaini kwamba lilifanya hivyo katika kulipiza kisasi kwa Urusi ambayo iliingilia kijeshi nchini Syria kwa kumsaidia Bashar Al Assad. "Lakini hatujui kwa kweli kama wanajihadi wenye msimamo mkali walihusika", ameongeza Clapper.

" Mara tu baada ya vinasa sauti vya ndege vitakua vimefanyiwa uchunguzi (...) labda tunaweza kujua zaidi ", amesema afisa huyo wa Marekani.

Maafisa wengine wa Marekani wamebaini pia kwamba ni vigumu wakati huu kufanya uhusiano na kitendo cha kigaidi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.