Pata taarifa kuu
VATICAN-AFRIKA-MARIDHIANO

Papa Francis: "naleta ujumbe wa maridhiano kwa Afrika"

Papa Francis anajianadaa kuanza ziara yake barani Afrika Jumatano wiki hii.
Papa Francis anajianadaa kuanza ziara yake barani Afrika Jumatano wiki hii. REUTERS/Giampiero Sposito

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani anatarajiwa kuanza ziara yake barani Afrika siku ya Jumatano juma hili.

Matangazo ya kibiashara

Nchi yake ya kwanza kuzuru itakuwa ni Kenya kati ya tarehe 25 hadi 27 na serikali ya Nairobi inasema maandalizi yamekamilika kumpokea kiongozi huyo.

Mamilioni ya watu wanatarajiwa kushiriki misa itakayoongozwa na Papa Francis jijini Nairobi.

Siku mbili kabla ya ziara hiyo, Papa Francis ametuma ujumbe wa tumaini kwa watu wa Afrika na kusema anawaletea ujumbe wa amani, msamaha na msamaha.

Baada ya Kenya, Papa Francis atazuru Uganda na kumalizia ziara yake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.