Pata taarifa kuu
VATICAN-PAPA-AFRIKA-MARIDHIANO

Changamoto za ziara ya Papa Francis barani Afrika

Papa Francis wakati wa Siku ya Maombi ya Kulinda viumbe katika Kanisa la Mtakatifu Petro Vatican, Septemba 1, 2015.
Papa Francis wakati wa Siku ya Maombi ya Kulinda viumbe katika Kanisa la Mtakatifu Petro Vatican, Septemba 1, 2015. REUTERS/Tony Gentile

Jumatano hii Novemba 25 asubuhi, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis atakua njiani kuelekea barani Afrika kwa ziara ya siku sita.

Matangazo ya kibiashara

Kwa muda wa siku hizo sita, Papa Francis ataanza ziara yake nchini Kenya, Uganda na hatimaye Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ziara hiyo inakumbwa na changamoto nyingi na inatokea hasa katika mazingira ambapo Makanisa ya Kiprotestanti yamekua mengi katika bara la Afrika.

Kabla ya ziara hiyo barani Afrika, Papa Francis hivi karibuni alitembelea kisiwa cha Lampedusa nchini Italia kilichoshuhudia wimbi la wakimbizi kutoka Afrika, huku Waafrika wengi wakiwa walipoteza maisha wakati walipokua wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean kuelekea Ulaya.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki hajawahi kutembelea Afrika hata wakati alikua bado hajateuliwa katika nafasi hiyo ya upapa, amearifu mwandishi wetu Vatican, Antoine-Marie Izoard.

Kutoka Nairobi hadi Bangui kupitia Kampala, kwa siku sita, Papa Francis atahubiri amani, mazungumzo kati ya dini na mapambano dhidi ya kutengwa. Licha ya kuhamasisha Kanisa Katoliki, hasa vijana wa Kikatoliki, Papa pia atafanya ziara kadhaa za ishara, kama ile ya kitongoji kikubwa chenye wakazi duni nchini Kenya, zahanati nchini Uganda, au kambi ya wakimbizi wa ndani na Msikiti jijini Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mjini Nairobi, Papa pia atatembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo anatazamiwa kuzungumzia kuhusu ulinzi wa dunia na mapambano dhidi ya kutengwa. Nchini Uganda, ataweka kipao mbele ushahidi wa imani ya mashujaa, Wakatoliki na Waanglikana, waliouawa katika karne ya 19.

"Ujumbe wa Amani"

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kama hali ya usalama itaruhusu, Papa Francis atahamasisha mjadala na maridhiano, huku kukiwa na mvutano baina ya jamii. "Natumaini kwa moyo wangu wote kwamba ziara yangu inaweza kuchangia kwa namna moja au nyingine kuponya majeraha yenu na kuanzishwa upya maisha ya baadaye kwa ajili ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na wakazi wake wote", Papa Francis amesema akiwahutubia raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenye Radio Vatican.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.