Pata taarifa kuu
SENEGAL-SIASA-MACKY SALL

Senegal: Macky Sall afuta nia yake ya kupunguza muda wa muhula wake

Rais wa Senegal Macky Sall, tarehe 1 Desemba 2015, katika mkutano kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (COP21) mjini Paris.
Rais wa Senegal Macky Sall, tarehe 1 Desemba 2015, katika mkutano kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (COP21) mjini Paris. © LOIC VENANCE / AFP

Rais wa Senegal Macky Sall ametangaza wakati wa hotuba iliyorushwa hewani kwenye runinga za Senegal Jumanne hii, Februari 16, kwamba, kulingana na ushauri wa Baraza la Katiba, ameamua kufuta nia yake ya kupunguza muda wa muhula wake unaoendelea kutoka miaka saba hadi mitano.

Matangazo ya kibiashara

Macky Sall amebaini kwamba atatuma rasimu yake ya marekebisho ya Katiba kwenye kura ya maoni tarehe 20 Machi ili raia wajiamuliwe wenyewe.

Macky Sall ametangaza kwamba muhula wake utakwenda hadi mwisho kwenye muda uliopangwa na Katiba, yaani hadi mwaka 2019.

"Katika utekelezaji wa kupunguza muda wa muhula wa rais unaoendelea, Baraza la Katiba linaona kwamba sheria hii inapaswa kufutwa, kwa madai kuwa si sambamba na haiwajibiki na Katiba ya sasa", Rais Macky Sall amesema, kabla ya kuongeza: "napaswa kukubaliana na uamuzi wa Baraza la Katiba. Matokeo yakeni kuwa muhula wa rais kwa sasa utakwenda hadi mwaka 2019. "

Katika hotuba yake, Macky Sall ameelezea chaguo lake. Chaguo la kisheria, kwani anapaswa kuheshimu Katiba na hasa Ibara ya 92, ambayo inamlazimisha kiongozi yeyote kuheshimu maamuzi ya Baraza la Katiba.

"Ibara ya 92 ya Katiba inanilazimisha kufanya hivyo. Ninanukuu: "maamuzi ya Katiba hayana muafaka wala kupingwa. Yanapingwa na uamuzi wa raia". Siwezi kwenda kinyume na na sheria hii", Rais wa Senegal amesema.

Hata hivyo, kuhusu kanuni ya jumla ya kupunguza muda wa muhula wa urais, Baraza la Katiba limekubali. Aidha, rais wa Senegal amesema kuwa kura ya maoni juu ya rasimu ya marekebisho ya Katiba "itafanyika Jumapili, Machi 20, 2016."

Lakini wakati wowote, kila baada ya dakika kumi ya hotuba yake, Macky Sall amekua akitaja ahadi yake, aliotoa kati ya duru mbili za uchaguzi wa rais wa mwaka 2012, ya kupunguza muda wa muhula wake kutoka miaka saba hadi tano.

Maoni ya wanasiasa na raia

Wawakilishi wa upinzani wa kisiasa na asasi za kiraia wamekataa kwenda kwenye televisheni na redio kutoa maoni yao.

Akihojiwa kwa njia ya simu, Fadel Barro, mmoja wa viongozi wanaharakati wa shirika la kiraia " Y'en a marre", amesema rais hakua na nia ya kupunguza muda wa muhula wake. "Macky Sall alikua na fursa ya kipekee ya kufunua ukurasa mpya. Kwa sasa ni fujo kwa nchi hii. "

Chama cha Abdoulaye Wade, cha PDS kimekumbusha kwamba "upinzani, ambao ni kiungo muhimu katika mfumo wa kisiasa nchini Senegal, haujawahi kuhusishwa katika mchakato wa mageuzi."

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.