Pata taarifa kuu
UINGEREZA-GAMBIA-USHIRIKIANO

Boris Johnson ahitimisha ziara yake nchini Gambia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Boris Johnson asifia utawala mpya wa rais wa Gambia Adama Barrow.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Boris Johnson asifia utawala mpya wa rais wa Gambia Adama Barrow. REUTERS/Darren Staples

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Boris Johnson, amemaliza ziara yake nchini Gambia, ambako amesifia utawala mpya wa rais Adama Barrow hasa baada ya kutangaza kurejea kwenye jumuiya ya nchi za Madola.

Matangazo ya kibiashara

Johnson alikutana na rais Barrow pamoja na waziri wake wa Mambo ya Ndani Mai Fatty, mkutano uliolenga kurejesha uhusiano wa nchi hizi mbili baada ya miaka kadhaa ya uhusiano tata chini ya kiongozi wa zamani Yahya Jammeh.

Ziara yake ilikuwa ni ya kwanza kufanywa na kiongozi wa juu wa Uingereza kwenye nchi hiyo ambapo anakuwa waziri wa mambo ya nje wa kwanza kuitembelea Gambia toka ilipopata uhuru wake mwaka 1965.

Gambia ilikumbwa na mgogoro wa kisasa baada ya rais Yahya Jammeh kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwezi Desemba 2016. Jammeh Aliondoka nchini Gambia baada ya kulazimishwa na jumuiya ya uchumi ya nchi za afrika Magharibi ECOWAS.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.