Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Basi la raia lalipuka katika mkoa wa Gossi

Kikosi cha jeshi la Ufaransa (Barkhane) chasaidia kuwasafirisha majeruhi wa shambulio dhidi ya basi la raia mkoani Gossi, nchini Mali, Februari 19, 2017.
Kikosi cha jeshi la Ufaransa (Barkhane) chasaidia kuwasafirisha majeruhi wa shambulio dhidi ya basi la raia mkoani Gossi, nchini Mali, Februari 19, 2017. @Barkhane

Basi lililokua lilisafirisha abiria kadhaa nchini Mali siku ya Jumapili lilikanyaga bomu la kutegwa ardhini na kulipuka, mtu mmoja alipoteza maisha na wengine 14 walijeruhiwa. Mlipuko huo ulitokea katika mkoa wa Gossi kusini magharibi mwa jimbo la Gao.

Matangazo ya kibiashara

Mara tu baada ya tukio hilo zoezi la uokoaji liliendeshwa kwa ulinzi mkal. Vikosi vya vya jeshi vya Mali, kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma) na kikosi cha Ufaransa nchini humo (Barkhane) vilitumwa katika eneo la tukio. Watu waliojeruhiwa bado wanapata matibabu katika jimbo Gao, lakini tisa miongpni mwa majeruhi wanaendelea vizuri lakini wengine watano ambao bado wanaendelea kutibiwa katika hospitali ya kijeshi ya Barkhane wako katika hali mbaya.

Mlipiko huo ilitokea mapema asubuhi Jumapili Februari 19 kwenye barabara itokayo Hombori kuelekea Gossi. Abiria kadhaa walikua ndani ya basi hilo.

Wakati huo huo serikali ya Mali iliomba msaada kutoka kwa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma) na Kikosi cha Ufaransa nchini humo (Barkhane) kutuma helikopta kadhaa na timu ya matabibu kwenye eneo la tukio.

Majeruhi walisafirishwa haraka hadi kilomita 150 katika mji wa mji wa Gao. Wale walioathirika zaidi wanapewa matibabu na jeshi la Ufaransa, na wengine wanahudumiwa na shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu. Baadhi yao wako katika mbaya, timu ya madaktari bingwa itawatembelea leo Jumatatu. "Hii ni hali isiyotarajiwa kwao, amesema Fortuna Katula, kaimu kiongozi wa ICRC katika jimbo la Gao.

"Tulituma helikopta tatu kwenye eneo la tukio na katika kila helikopta walikuemo askari 22 ikiwa ni pamoja na timu za matabibu ili kuhudumia watu waliojeruhiwa, " amesema Luteni Kanali Philippe, msemaji wa kikosi cha Ufaransa nchini Mali (Barkhane).

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.