Pata taarifa kuu
GAMBIA-SIASA

Raia wa Gambia wanapiga kura kuwachagua wabunge

Raia wa Gambia wakisubiri kupiga kura
Raia wa Gambia wakisubiri kupiga kura rfi

Raia wa Gambia wanapiga kura siku ya Alhamisi kuwachagua wabunge baada ya ule wa urais mwaka uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Huu ni uchaguzi wa kwanza kufanyika chini ya serikali mpya ya rais Adama Barrow na baada ya kuondoka nchini humo kiongozi wa zamani Yahya Jammeh, aliyeongoza nchi hiyo kwa miaka 22.

Vyama tisa vinashiriki katika Uchaguzi huu, kikiwemo chama cha Jammeh APRC.

Chama cha rais Barrow UDP ambacho kimeungana na vyama vingine vodogo vidogo, kinatafuta ushindi katika uchaguzi huu.

Mgombea wa urais Mama Kandeh aliyemaliza katika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa urais, naye anaonekana kuwa na ushawishi kupitia chama cha GDC.

Wapiga kura wa Gambia 880,000 wanashiriki katika zoezi hili linalotarajiwa kumalizika saa 11 jioni saa za Banjul.

Wabunge 53 wanatarajiwa kuchaguliwa katika uchaguzi huu kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi nchini humo IEC.

Katiba ya Gambia inampa mamlaka rais wa nchi hiyo kuteuwa wabunge wengine watano, na hivyo kulifanya bunge la nchi hiyo kuwa na wabunge 58.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.