Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALAMA-UCHAGUZI

Uchaguzi wa urais Ufaransa: Duru ya kwanza kufanyika chini ya ulinzi mkali

Zaidi ya polisi 50 000 watatumwa kwa ushirikiano na askari 7000 kuimarisha usalama katika maeneo mbalimbali, Jumapili Aprili 23 wakati wa uchaguzi wa rais.
Zaidi ya polisi 50 000 watatumwa kwa ushirikiano na askari 7000 kuimarisha usalama katika maeneo mbalimbali, Jumapili Aprili 23 wakati wa uchaguzi wa rais. REUTERS/Charles Platiau

Siku moja baada ya shambulio lililotokea kwenye mtaa wa Champs Elysées, mjini Paris, nchini Ufaransa, ambapo polisi mmoja aliuawa na wengine wawili kujeruhiwa, serikali ya Ufaransa imechukua hatua kali za usalama. Hayo yanajiri wakati ambapo zimesalia siku chache tu ili uchaguzi wa urais ufanyike Jumapili Aprili 23.

Matangazo ya kibiashara

Baada mkutano wa Baraza la Ulinzi lililokutana Ijumaa asubuhi chini ya uwenyekiti wa François Hollande, Waziri Mkuu Bernard Cazeneuve alisema "hakuna kitakacho zuia uchaguzi kufanyika ".

Polisi zaidi ya 50,000 na kitengo kikingine cha polisi kitakachosaidiwa na askari 7000 wa kikosi cha Ulinzi kitatumwa siku ya Jumapili ili kuimarisha usalama kwa ajili ya uchaguzi katika vituo vya kupigia kura 60,000.

Waziri wa Mambo ya Ndani Matthias Fekl alibainisha, hata hivyo, kwamba hakuna askari au polisi ambaye ataonekana katika kituo cha kupigia kura.

"Ni sheria ya kidemokrasia," amesema Matthias Fekl. Ametoa agizo kwa Mameya wa miji kwamba kila kiongozi wa kituo cha kupigia kura anatakiwa kuwa na namba ya simu ya moja kwa moja kwa vikosi vya usalama.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.