Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA

Macron yupo nchini Mali kuzindua kikosi cha Sahel

Rais wa Ufaransa  Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron REUTERS/Christophe Archambault

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaungana na marais kutoka mataifa matano ya Sahel ya Mauritania, Mali, Burkina Faso, Niger na Chad jijini Bamako, kuzindua kikosi maalum cha wanajeshi 5,000 kupambana na makundi ya kijihadi katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Rais Macron, anatarajiwa kuwahakikishia viongozi hao wa Afrika uungwaji mkono na ushirikiano wa karibu katika vita dhidi ya Uganda.

Aidha, anatarajiwa kuomba msaada kutoka Ujerumani, Uholanzi, Ubelgiji na Marekani kutoa mchango zaidi wa Euro Milioni 50 kufanikisha operesheni hiyo.

Viongozi hao pia wanatarajiwa kuja na mbinu ya wanajeshi zaidi ya 4,000 wa Ufaransa watakavyoondoka katika eneo la Sahel na kuwaachia operesheni hii kwa kikosi hiki kipya.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinikisha kikosi hicho.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.