Pata taarifa kuu
SENEGAL-SIASA-UCHAGUZI

Chama tawala chapata viti vingi bungeni nchini Senegal

Wafuasi wa rais Macky Sall wakati wa kampeni za uchaguzi wa wabungeJulai 30, 2017 nchini Senegal.
Wafuasi wa rais Macky Sall wakati wa kampeni za uchaguzi wa wabungeJulai 30, 2017 nchini Senegal. SEYLLOU / AFP

Chama tawala nchini Senegal kimejipatia ushindi katika uchaguzi wa Bunge uliofanyika Jumapili iliyopita na hivyo kudhibiti wingi wa viti katika Bunge la nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mahammed Abdallah Dionne Waziri Mkuu wa Senegal sambamba na kutangaza ushindi wa muungano unaomuunga mkono rais Macky Sall wa nchi hiyo amesema kuwa, muungano huo umefanikiwa kujikusanyia wingi wa kura katika miji 45 ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Muungano unaoongozwa na Khalifa Sall, Meya wa mji wa Dakar, ambaye anazuiliwa jela umeshika nafasi ya pili ukifuatiwa na muungano ulioundwa na Abdoulaye Wade, rais wa zamani wa Senegal.

Hata hivyo wapinzani nchini humo wanaitaja hatua hiyo kwamba, ilikuwa na malengo ya kisiasa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.