Pata taarifa kuu
ANGOLA-UCHAGUZI-SIASA

Rais mpya wa Angola kutawazwa Jumnne hii

Picha ya João Lourenço wakati wa kampeni ya uchaguzi.
Picha ya João Lourenço wakati wa kampeni ya uchaguzi. AMPE ROGERIO / AFP

Rais mpya wa Angola João Lourenço ataapishwa Jumanne hii 26 Septemba kama Rais mpya wa Angola. Anachukua hatamu ya uongozi wa nchi baada ya miaka 38 ya utawala wa José Edouardo Dos Santos.

Matangazo ya kibiashara

Joao Lourenço, afisa wa ngazi ya juu katika jeshi aliyestaafu, alichaguliwa hivi karibuni baada ya kuchaguliwa katika chama tawala cha MPLA kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti. Ushindi wa chama cha tawala cha MPLA katika uchaguzi mkuu wa Agosti ulithibitisha ukurasa mpya wa taifa hilo, ambalo liliongozwa na Dos Santos kwa muda wa miaka 38.

João Lourenço, aliyekuwa waziri wa ulinzi anachukuwa nafasi ya Jose Eduardo Dos Santos rais anayeondoka ambaye aliamua kuachia madaraka baada ya kuongoza miaka thalathini na nane.

Vyanzo rasmi vinaeleza kuwa ushawishi wa José Edouardo Dos Santos utaendelea kuwepo. Rais wa zamani ataendelea kuongoza chama cha MPLA hadi mwaka 2022. Lakini chama hiki bado ni taasisi muhumi katika maamuzi ya nchi.

Familia ya Dos Santos itaendelea kudhibiti Angola. Isabel, binti yake, anasimamia kampuni ya mafuta ya kitaifa ya Sonangol, ambayo inaingiza 70% ya mapato ya bajeti. Jose Filomeno, mwanawe wa kiume, anasimamia Mfuko mkuu uliozindua kuendeleza nchi ya Angola.

Watoto wengine wawili wanasimamia kampuni kuu ya uzalishaji na matangazo nchini Angola. Hatimaye, mke wa José Edouardo Dos Santos ana makampuni katika sekta ya benki na almasi.

Wengi sasa wanasubiri kuona watu watakaounda serikali yake serikali na jinsi itatumia mamlaka muhimu ambayo Katiba inaipa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.