Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFRIKA-USALAMA

Marekani kutoa dola milioni 60 kusaidia kikosi cha kikanda cha G5 Sahel

Mkutano wa G5 Sahel Julai 2, 2017, Bamako.
Mkutano wa G5 Sahel Julai 2, 2017, Bamako. CHRISTOPHE ARCHAMBAULT / AFP

Marekani imeahidi kutoka dola za Marekani milioni 60 kusaidia mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi katika mataifa ya Sahel barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Marekani imekataa ombi la Ufaransa na Mataifa ya Afrika, kukabidhi kazi hiyo kwa Umoja wa Mataifa.

Marekani imeahidi kutoa msaada huo wa fedha kupitia Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tllerson wakati wa mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Ufaransa imekuwa katika mstari wa mbele kusaidia jeshi la pamoja kutoka Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania na Niger kupambana na makundi hayo ya kijihadi.

Ufaransa ambayo iliongoza kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hakufaulu kumshinikiza mshirika wake Marekani kuhusu Umoja wa Mataifa kuingilia suala la mdororo wa usalama katika ukanda wa Afrika Magharibi, licha ya kutaka kikosi cha kikanda cha G5 Sahel kusaidiwa kwa fedha na vifaa.

Katika kikao cha siku ya Jumatatu (Oktoba 30) kilichofanyika kuhusu msaada wa Umoja wa Mataifa kwa kikosi hiki cha kikanda chenye lengo la kupambana dhidi ya ugaidi, Marekani ilikubali kutoa msaada wa dola milioni 60.

Hata hivyo Marekani bado inakataa kupitisha ombi la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, nchi tano za Sahel, Ufaransa na nchi nyingi wananchama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kuidhinisha msaada wa Umoja wa Mataifa kwa kikosi hiki. Ufaransa inachunguza, hata hivyo, kwamba kumekuwa na na uingiliaji katika msimamo wa Marekani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.