Pata taarifa kuu
SAHEL-UFARANSA-UNSC-UGAIDI-USALAMA

Ufaransa yaomba Umoja wa Mataifa kusaidia kikosi cha G5 Sahel

Askari wa kikosi cha G5 Sahel katika eneo la In Tillit, Mali wakati wa operesheni yao ya kwanza, Hawbi, mapema mwezi Novemba 2017.
Askari wa kikosi cha G5 Sahel katika eneo la In Tillit, Mali wakati wa operesheni yao ya kwanza, Hawbi, mapema mwezi Novemba 2017. RFI / Anthony Fouchard

Ufaransa inalitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuruhusu jeshi la Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA, kusaidia jeshi la Afrika katika mapigano dhidi ya makundi ya kigaidi katika eneo la Sahel.

Matangazo ya kibiashara

Paris imewasilisha azimio katika Baraza hilo kuomba msaada huo bila ya bajeti yake kuongezeka.

Marekani imeahidi kutoa Dola za Marekani Milioni 60 kusaidia opereshni hiyo inayoleta wanajeshi kutoka Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania na Niger waliounda kikosi cha pamoja.

Uongozi wa kikosi hiki unaundwa kwa sasa na jenerali mmoja kutoka Nigeria, mkuu wa majeshi kutoka Chad na afisa mwengine wa jeshi kutoka Cameroon. Taratibu za uendeshaji na sheria za ushiriki zilipitishwa miezi kadhaa iliopita.

Nigeria na majirani zake wamekuwa wanajitahidi kupambana na wapiganaji wa Boko Haram ambao wameua watu zaidi ya elfu ishirini katika Ukanda huo wa Afrika Magharibi.

Hivi karibuni Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitolea wito kwa jumuiya ya kimataifa kuzitolea msaada wa kifedha nchi za Nigeria, Cameroon, Chad, Niger na Benin, nchi ambazo zinachangia kuundwa kwa kikosi hiki chenye lengo la kupambana na kundi la Islamic State katika Afrika magharibi (Boko Haram).

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.