Pata taarifa kuu
DRC-HRW-M23-USALAMA

DRC yakanusha ripoti ya Human Right Watch kuhusu M23

Wapiganaji wa kundi la zamani la waasi la M23 mbele ya kambi ya Ramwanja, Desemba 17, 2014.
Wapiganaji wa kundi la zamani la waasi la M23 mbele ya kambi ya Ramwanja, Desemba 17, 2014. AFP PHOTO/ ISAAC KASAMANI

Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Right Watch limemtuhumu rais Joseph Kabila wa DRC kuwasajili wapiganaji wa zamani wa kundi la M23 kwa lengo la kuwakandamiza waandamanaji waliokuwa wakipinga utawala wake Desemba 19 na 20 mwaka 2016 jijini Kinshasa.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika hilo, ukandamizaji zilisababisha vifo vya watu 60.

Serikali ya DR Congo kupitia waziri wake wa haki za binadamu Marie Ange Mushobeka, amesema ameshangazwa na ripoti hiyo na kwamba shirika hilo halina ushahidi wowote kuhusu tuhuma hizo.

Hata hivyo Human Wright Watch inasema ilikusanya ushahidi kupitia watu mbalimbali wakiwemo wapiganaji hao waliotoa ushuhuda kama anavyoeleza hapa Ida Soyere mkurugenzi wa Human Right Watch katika ukanda wa Afrika ya kati.

Upande wake Waziri wa Ulinzi nchini DR Congo, Crispin Atama Thabe, amesema tuhuma hizo zimekuja ili kulichafuwa jeshi na kuharibu uaminifu na kwamba, wakati wa mapigano dhidi ya kundi hilo maafisa kadhaa wa FARDC walipoteza maisha, hivyo hawana sababu ya kuwatumia wanajeshi hao.

Naye kiongozi wa zamani wa kundi la M23 Bertrand Bisimwa amesema serikali ya Congo imewaajiri kupitia mlango wa nyuma wapiganaji wa zamani walioasi kundi hilo waliofukuzwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.