Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Waziri Mkuu wa Mali ajiuzulu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2018

Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita
Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita REUTERS/Benoit Tessier

Waziri Mkuu wa Mali Abdoulaye Idrissa Maiga pamoja na Mawaziri wake, wamejiuzulu.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imetolewa na Ofisi ya rais jijini Bamako, bila ya kutoa ufafanuzi wowote.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema huenda Maiga anajiandaa kuwania urais mwaka ujao dhidi ya rais Ibrahim Boubacar Keita.

Hata hivyo kuna wale wanaosema kuwa amaejiuzuli ili kuongoza Kamati ya kampeni kumsaidia rais Keita kama ilivuokuwa mwaka 2013.

Rais Keita anatarajiwa kumteua Waziri Mkuu mpya hivi karibuni.

Serikali mpya ya rais Keita itakuwa ya tano tangu mapinduzi ya kijeshi nchini humo miaka minne iliyopita.

Maiga alikuwa Waziri Mkuu wa nne baada ya Oumar Tatam Ly ,Moussa Mara na Modibo Keita.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.