Pata taarifa kuu
SOMALIA-HRW-AL SHABAB-USALAMA

Human Right Watch yaishtumu Al Shabab kuajiri watoto Somalia

Wakimbizi wa Somalia, hapa ilikua Desemba 19, 2017.
Wakimbizi wa Somalia, hapa ilikua Desemba 19, 2017. REUTERS/Baz Ratner

Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Right Watch, katika ripoti yake mpya, limeshtumu kundi la wapiganaji wa Kiislamu nchini Somalia kuendelea kuajiri watoto nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Human Right Watch wanamgambo wa kundi la Al Shabab wanaendelea kutishia raia kwa kuwalazimisha kutoa vijana wao kwa kulipigania kundi hilo. Katika uchunguzi wake, Human Right Watch limesema mamia ya vijana walilazimika kujiunga na kundi hili la kigaidi.

Ripoti ya HRW inaelezea watoto, wakati mwingine wenye umri wa miaka minane, ambao wanatolewa kwa nguvu katika familia zao na kisha kuingizwa katika shule kubwa za dini zinazomilikiwa na kundi la Al Shabab. Katika shule hizo wanalazimishwa kufuata itikadi za kigaidi na mara nyingi kuwa hata wapiganaji.

Kundi la Al Shabab limewachukua au kuwateka watoto kwa kipindi cha miaka mingi. Kabla kundi hili lilikua likifanya hivyo hasa katika maandalizi ya vita, hasa kwa kuwafanya kama ngao zao kwa vita. Lakini kwa upande wa Laetitia Bader, ambaye alifanya uchunguzi huo, anasema inawezekana kuwa wakati huu kundi la Al shabab limeamua kutumia njia nyingne. Jamii nyingi, hasa masikini, haziwezi tena kulipa kodi zilizowekwa na kundi la Al Shabab. Hasa kwa sababu ya ukame. Hivyo basi kundi hili la kigaidi linatumia watoto kama kodi.

Pia ni njia ya kundi hili kuendeleza utawala wake kwa raia. Kwa hili, wapiganaji wa Al Shabab wamekua wakiendesha mashambulizi katika vijiji mbalimbali na kuwateka nyara watoto. Au wanatoa shinikizo kwa viongozi wa makabila, kwa kuwatishia kifo, kuwapa muda wa mwisho ili raia watoe vijana wao wa kiume na wa kike.

Kwa hali hii, raia wameamua kutuma vijana wao katika miji, mbali na maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Al Shabab. "Wazazi wengi wanafikiri ndiyo njia pekee ambayo wanaweza kuwa salama," amesema Laetitia Bader. Lakini safari kwenda mijini ni hatari kwa vijana hawa wasio na msaada. Wanakokwenda huko hupokelewa na ndugu kutoka familia zao, wengine wamekua wakiomba hifadhi katika makambi ya wakimbizi wa ndani. Wakati mwingine, wakazi pia wanaamua kuweka miradi ya kuwasaidia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.