Pata taarifa kuu
AFYA

Utafiti: Wanawake kupata hedhi chini ya miaka 12 kunasababisha magonjwa ya moyo

Daktari akiwa kwenye maabara
Daktari akiwa kwenye maabara REUTERS/Chris Radburn

Utafiti mpya wa kitabibu uliochapishwa hii leo umeonesha kuwa wanawake ambao wanaanza kupata hedhi katika umri wa miaka 11 au kabla na kufikia ukomo wa kupata hedhi kabla ya miaka 47, wako hatarini kupata magonjwa ya moyo na kupooza.

Matangazo ya kibiashara

Utafiti huu umebaini kuwa mimba kuharibika, kujifungua mtoto aliyekufa baada ya kukamilika kwa majuma 24 ya mimba, operesheni za kuondoa ukuta wa kizazi na kubeba mimba katika umri mdogo pia kumehusishwa na mtu kupata magonjwa ya moyo kwenye umri mkubwa.

Hata hivyo wataalamu hao wameonya kuwa, hii si mara ya kwanza kugundulika kwa uhusiano kati ya visababishi vya uzazi na magonjwa ya moyo na kwamba takwimu hazioneshi uhusiano wa kawaiada.

Wanasayansi walichuku takwimu kutoka katika utafiti wa muda mrefu nchini Uingereza ambao ulifuatilia na kuwapima zaidi ya wanawake robo milioni kati ya mwaka 2006 na 2016, ambapo wastani wa umri wa wanawake waliofanyiwa vipimo ulikuwa ni miaka 56.

Zaidi ya watu laki nne hadi laki tano walikuwa wajawazito na karibu nusu yao walikuwa na watoto wawili, kwa wastani hii inamaanisha walianza kupata hedhi wakiwa na umri wa miaka 13 na watoto wao wa kwanza katika umri wa miaka 26.

Katika mwaka 2016, mbili ya tatu ya wanawake walipitia kipindi cha kukoma hedhi katika wastani wa umri wa miaka 50.

Utafiti umeonesha kuwa wanawake walioanza kupata hedhi kabla ya umri wa miaka 12, asilimia 10 kati yao walikuwa kwenye hatari ya kupata matatizo ya moyo ukilinganisha na wale waliokuwa na umri wa miaka 13 na zaidi.

Kwa wanawake waliofikia ukomo wa hedhi chini ya miaka 47 hatari ya kupata magonjwa ya moyo iliongezeka kwa asilimia 33 na kupooza peke yake ilikuwa ni asilimia 42.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.