Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mlipuko waua watu 26 Mali

Eneo la Boni linapatikana katika mkoa wa Mopti, katikati ya Mali.
Eneo la Boni linapatikana katika mkoa wa Mopti, katikati ya Mali. AFP PHOTO/John Macdougall

Watu 26 raia wa Mali na Burkinafaso wamepoteza maisha wakiwemo wanawake na watoto baada ya gari walililokuwa wanasafiria kukanyaga bomu la kutegwa ardhini katika mji wa Boni katikatika ya nchi ya Mali.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa hakuna abiria hata mmoja aliyenusurika na mashuhuda wanasema ni vigumu kuwatambua watu waliopoteza maisha kwa sababu miili yao imekatikakatika.

Awali watu waliokuwa wameripotiwa kuppoteza maisha ilikuwa ni 13, wakiwemo watito wanne na mama zao.

Ripoti zinasema kuwa, gari hili lilikuwa limetoka nchini Burkina Faso kwenda kuwapeleka wafanyibiashara katikati mwa nchi ya Mali.

Magaidi wamelaumiwa kwa kuzika vilipuzi hivyo ardhi kwa lengo la kusababisha maafa ya raia.

Makundi ya wapiganaji wa kijhadi yananyooshewa kidole huenda ndio waliohusika na utegaji wa bomu hilo.

Matukio ya aina hiyo yamekuwa yakishuhudiwa katika maeneo hayo, lakini yamekuwa yakiwalenga wanajeshi, ni mara ya kwanza inatokea kwa raia wa kawaida.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.