Pata taarifa kuu
SENEGAL-AJALI-HELIKOPTA

Ajali ya helikopta nchini Senegal yasababisha maafa

Ajali ya helikopta nchini Senegal Machi 15 2018
Ajali ya helikopta nchini Senegal Machi 15 2018 eaace.com

Watu wanane wameuawa na 12 kujeruhiwa nchini Senegal baada ya helikopta ya kijeshi kuanguka nchini Senegal.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa ajali hiyo imetokea katika eneo la Missirah, katika  mpaka wa Kaskazini karibu  na nchi ya Gambia.

Helikopta hiyo ilikuwa inawasafirisha watu 20 waliokuwa wanarejea nyumbani baada ya kuhudhuria mazishi katika eneo la Ziguinchor, Kusini mwa jiji kuu Dakar.

Rais Macky Sall, ametuma risala za rambirambi kwa jamaa ndugu na marafiki wa watu waliopoteza maisha na kuagiza uchunguzi kufanyika kubaini kilichosababisha ajali hiyo.

Mara ya mwisho kutokea kwa ajali ya ndege nchini Senegal ilikuwa ni mwaka 2015, wakati abiria saba walipopoteza maisha baada ya kupata ajali.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.