Pata taarifa kuu
BURUNDI

Burundi: Kura ya maoni kuhusu katiba kufanyika Mei 17

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. REUTERS/Evrard Ngendakumana

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza hapo jana ametia saini sheria tata inayotoa wito kwa wananchi wa taifa hilo wenye umri wa kupiga kura ya maoni juu ya marekebisho ya katiba ambayo yanaweza kumruhusu kuendelea kukaa madarakani hadi mwaka wa 2034 kushiriki kwenye kura hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Rais huyo mwenye umri wa miaka 54 ambae yupo madarakani tangu mwaka 2005, sasa anataka kuendelea kusalia kwenye nafasi hiyo hadi mwaka 2035.

Sheria hiyo ya mabadiliko ya katiba ya Burundi inasema mabadiliko yataidhinishwa iwapo asilimia 50 ya kura za ndio na kura moja itafikiwa.

Hata hivyo upinzani unasema alichokifanya rais Nkurunziza kinakwenda kinyume na katiba ya nchi, maana mabadiliko ya katiba ili yaidhinishwe, lazima yapitie katika mabaraza ya bunge na seneti.

Wale wote wanaohitaji kuendesha kampeni ya ndio au hapana kuhusu mabadiliko ya katiba wamepewa muda wa hadi April 6 kujiorodhesha kwa tume ya uchaguzi ambapo kampeni imepangwa kuanza majuma mawili kabla ya terehe ya kupiga kura.

Inaelezwa kuwa watu kadhaa wako korokoroni kwa tuhuma za kuendesha kampeni ya hapana kabla ya wakati.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.