Pata taarifa kuu
UN-DRC

UN yaonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu nchini DRC

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura.
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura. UN Photo/Loey Felipe

Baraza la usalama la umoja wa Mataifa limeonya kuwa hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeendelea kuwa mbaya na imefikia hatua ya kuwa janga kwenye baadhi ya maeneo ya nchi, huku mamilioni ya watu wakikabiliwa na njaa.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa DRC zaidi ya milioni 13 wanahitaji misaada ya kibinadamu wakiwemo watu milioni 7 na laki 7 ambao wana uhaba mkubwa wa chakula, imesema taarifa ya siri kwenye umoja wa Mataifa.

taarifa hiyo imesema kuwa hali mbaya ya kibinadamu imeongezeka mara mbili zaidi katika kipindi cha mwaka uliopita ambapo mamilioni ya raia wa DRC wamekimbia machafuko na wanakadiriwa kufikia milioni 4 na laki 4 kwa sasa.

Nchi wanachama za baraza la usalama zimeeleza kuguswa nakuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu ambayo sasa imefikia hatua ya kuogofya kwenye baadhi ya maeneo ya nchi.

Baraza hilo limeeleza umuhimu wa kushughulikia tatizo la makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo na kurejea wito wake wa kuwepo kwa uchaguzi ulio huru na haki.

Mamlaka mjini Kinshasa zimetangaza tarehe 23 ya mwezi Desemba mwaka huu kuwa tarehe rasmi ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, lakini hadi sasa bado haieleweki ikiwa rais Joseph Kabila hatowania tena uchaguzi huo ili kupisha mabadilishano ya mdaraka ya amani baada ya kumaliza mihula yake.

Maofisa wa umoja wa Mataifa wameeleza hofu ya nchi hiyo kutumbukia kwenye machafuko wakati huu tarehe za kuelekea kwenye uchaguzi zikikaribia.

Mkutano wa kimataifa utafanyika mwezi ujao mjini Geneva kwa lengo la kuhamasisha upatikanaji wa kiasi cha dola za Marekani bilioni 1 na laki 7 ili kusaidia hali ya kibinadamu nchini DRC, hii ikiwa ni kiasi ambacho ni mara nne ya kile kilichokusanywa mwaka uliopita.

Umoja wa Mataifa umetangaza hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuwa katika ngazi ya 4, ngazi ya juu zaidi ya UN kuhitajika misaada ya dharula.

Kwenye mkutano huo ulioripotiwa kufanyika siku ya Jumatatu, mkuu wa shirika la maendeleo la Marekani Mark Green alisema Serikali ya rais Kabila haijafanya vya kutosha kuondoa madhila yanayowakabilia wananchi wake.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.