Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Padri Havugimana Ngango atekwa nyara mashariki mwa DRC

Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco) kikipiga doria katika Hifadhi ya wanyama ya Virunga, Mashariki mwa DRC.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco) kikipiga doria katika Hifadhi ya wanyama ya Virunga, Mashariki mwa DRC. REUTERS/Kenny Katombe

Padri Havugimana Ngango Célestin amethibitishwa kutekwa nyara na waasi wasiojulikana siku ya Jumapili jioni katika maeneo ya Kihondo wilayani Ruchuru, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Mashahidi wanasema Padri Ngango alitekwa nyara na waasi wasio julikana akiwa kwenye gari lake kwenye barabara inayoelekea Kihondo katika eneo la Nyarukwangara ambako alisherehekea pasaka.

Waasi walimlazimisha kuondoka katika gari lake na kuwalazimisha Wakristu waliokua waliandamana nae kuondoka haraka eneo hilo, kwa mujibu wa mwanaharakati wa haki za binadam Liberate Buratwa.

“Inabidi raia wasimame kwani tumechoshwa na utekaji nyara na hao watoto sio wageni ni wakongomani na sisi wana wake tunajitahidi katika juhudi za kutokomeza utekaji nyara huo, “ amesema Liberate Buratwa.

Mbunge Bariyanga Rutuye aliyechaguliwa katika wilaya ya Ruchuru anasema hadi sasa waasi hao wanadai fidia ya dola laki tano.

“Tulijaribu kumtafuta, na kuna simu ambayo ilikua ikituita ambapo wanaomba dola laki tano, yaani nusu ya dola milioni moja ni huzuni sana, lakini kwa sasa raia pamoja na wanajeshi wapo wanajaribu kumtafuta..

Mwanzoni mwa mwaka huu Padri mmoja alitekwa nyara na kundi la waasi ambalo halikujulikana.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanaomba serikali ya DRC kufanya kazi yake ya kulinda raia ipasavyo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.