Pata taarifa kuu
MALI-UN-USALAMA

Mali: Kambi ya Minusma yashambuliwa Kidal

(Picha ya zamani) Jenerali Michael Lollesgaard (katikati), aliyekuwa Mkuu wa kikosi cha Walinda amani nchini Mali, hapa akizuru Aguelhok mnamo Septemba 13, 2016.
(Picha ya zamani) Jenerali Michael Lollesgaard (katikati), aliyekuwa Mkuu wa kikosi cha Walinda amani nchini Mali, hapa akizuru Aguelhok mnamo Septemba 13, 2016. RFI/Anthony Fouchard

Askari wawili wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma) waliuawa na wengine 10 walijeruhiwa siku ya Alhamisi (Aprili 5) katika shambulio dhidi ya kambi ya Minusma huko Aguelhok, kaskazini mwa Kidal, tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma) imesema.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa chanzo cha jeshi la Afrika kutoka Minusma huko Aguelhok, risi zilifyatuliwa kutoka eneo la mashariki mwa kambi ambapo kulionekana kundi la watu mapema mchana.

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali "nakumbusha kwamba mashambulizi dhidi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa yanaweza kuchukuliwa kama uhalifu wa kivita chini ya sheria ya kimataifa na kwamba wahusika wanaweza kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria vya kimataifa".

Minusma imethibitisha uamuzi wake wa "kusaidia juhudi za kurejesha amani na usalama wa kudumu nchini Mali".

Wakati huo huo, watu wanne waliokua kwenye pikipiki walishambulia kituo cha polisi siku ya Alhamisi katika jimbo la Mopti katikati mwa Mali bila kusababisha hasara, kwa mujibu wa chanzo cha polisi nchini Mali.

Si mara ya kwanza kambi ya kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali kushambuliwa. Mapem amwezi Januari 2016 kambi ya Minusma ilishambuliwa kwa makombora na kusababisha kifo cha askari mmoja

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.