Pata taarifa kuu
DRC-HAKI

Majaji wawili wa Mahakama ya Katiba wajiuzulu DRC

Mji mkuu wa DRC, Kinshasa.
Mji mkuu wa DRC, Kinshasa. Wikimedia/Moyogo

Majaji wawili wa Mahakam ya Katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamejiuzulu kwenye nafasi zao, na wamesalia majaji sita badala ya tisa.

Matangazo ya kibiashara

Jaji mmoja alifariki dunia siku ya Jumapili Aprili 8 na wengine wawili wamejiuzulu bila hata hivyo kutoa maelezo au sababu ya kujuzulu kwao. Uamuzi huu wa kujiuzulu kwa majaji hawa ilichukuliwa siku ya Jumatatu wiki hii, ikiwa imesalia miezi minane tu kabla ya uchaguzi.

Tangazo hilo lilimeishangaza serikali ya DRC, hata kama majaji hawa wawili walionyesha zaidi ya mara moja maoni tofauti na rais wa mahakama hiyo.

Mnamo Oktoba 17, 2016, Jean-Louis Esambo na Banyaku Luape hawakuripoti katika Mahakama ya Katiba, ambayo ambayo ingelitoa uamuzi muhimu kwa hatima ya DRC. Kutoa au la ruhusa kwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (Ceni) kuahirisha uchaguzi wakati ambapo muda uliwekwa kikatiba na kuongeza muhula wa pili na wa mwisho kwa Rais Kabila.

Kwa jumla, ni majaji wanne ambao walikataa kushiriki kikao hicho. Idadi ya majaji kulingana na sheria inayounda Mahakama ya Katiba haikukamilika, lakini Mahakama iliamua kuvunja sheria na kuidhinisha uchaguzi kuahirishwa kutokana na ombi lililotolewa na Ceni. Mkuu wa Mahakama alijaribu kuwataka wenzake kujielezea kwanini hawakushiriki kikao hicho, na kumpa kopi Rais Kabila.

Tangu wakati huo, kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, mvutano uliongezeka kati ya majaji mbalimbali wa Mahakama.

Jean-Louis Esambo na Banyaku Luape hawajaelezea waziwazi sababu za kujiuzulu. nafasi zao zitarejelewa na majaji wengine, ambapo mmoja atateuliwa na Bunge na mwengine atateuliwa na Baraza la Taifa la majaji. Jaji Kalonda ambaye alifariki juma lililopita, nafasi yake itarejelewa na jaji ambaye atateuliwa na Rais Kabila.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.