Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA-UN-MAGAIDI

Magaidi 15 wauawa nchini Mali baada ya kuwashambulia wanajeshi wa UN

Mwanajeshi wa kulinda amani nchini Mali
Mwanajeshi wa kulinda amani nchini Mali www.rfi.fr

Ufaransa inasema magaidi 15 wameuawa katika mji wa Kihistoria wa Timbukutu Kaskazini mwa Mali, baada ya uvamizi katika kambi ya wanajeshi wa kulinda amani.

Matangazo ya kibiashara

Uvamizi huo ulisababisha kifo cha mwanajeshi mmoja wa kulinda amani wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo (MINUSMA) baada ya kurushwa kwa vilipuzi katika kambi hiyo.

Taarifa za kijeshi nchini Ufaransa zinasema, wanajeshi wake saba walijeruhiwa.

Hii ndio mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kushambuliwa katika mji wa Timbukutu.

Katika uvamizi huo askari saba wa Ufaransa kutoka kikosi Barkhane alijeruhiwa.

Uvamizi huo ulifanyika katia kambi ya kikosi ha Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA) na kambi ya kikosi cha askari wa Ufaransa Barkhane.

Mashambulizi hayo yalidumu saa nne na magadi walikua walijihami vya kutosha, kwa mujibu wa msemaji wa kikosi cha askari wa Ufaransa, Barkhane.

Kwa upande wa Minusma kama upande wakikosi cha Ufaransa, wamebaini kwamba wamefaulu kuzima mashambulizi hayo. " Hata hivyo, mfumo wetu wa ulinzi umefanya kazi," chanzo cha Minusma kimesema.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.