Pata taarifa kuu

Kiongozi wa waasi wa zamani Liberia ahukumiwa miaka 30 jela Marekani

Kiongozi wa zamani wa waasi nchini Liberia, Mohammed Jabatteh amehukumiwa kifungo cha miaka 30, kwa kosa la kudangaya mamlaka.
Kiongozi wa zamani wa waasi nchini Liberia, Mohammed Jabatteh amehukumiwa kifungo cha miaka 30, kwa kosa la kudangaya mamlaka. Getty Images/ Spaces Images

Mahakama ya Marekani imemhukumu kiongozi wa zamani wa waasi Mohammed Jabatteh kifungo cha miaka 30. "Jungle Jabbah", jina lake la utani wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, alipatikana na hatia ya kudanyanya mamlaka kuwa alipewa hifadhi nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Mohammed Jabatteh, 51, ambaye ni baba wa familia na kiongozi wa kampuni moja nchini humo, alikamatwa mnamo mwezi Aprili 2016 wakati alipokua akiishi Philadelphia kufuatia mashitaka ya uongo na udanganyifu kwa mamlaka ya Marekani.

Alichokifanya sio uongo, lakini ni uhalifu kama mmoja wa viongozi wa makundi ya waasi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe (1989-2003) nchini Liberia, maafisa wa mahakama wamesema.

Mnamo mwezi Oktoba 2017, mashahidi zaidi ya kumi na tano waliitwa mahakamani ili kuja kutoa ukweli kuhusu maovu waliotendewa. Kwa muda wa majuma mawili kesi hiyo ikisikilizwa, tuhuma za mauaji, kuajiriwa kwa askari wa watoto, ubakaji, na uharibifu vilitajwa.

Kesi isio ya kawaida kwa waathirika wa uhalifu wa vita nchini Liberia, ameelezea Alain Werner, mkurugenzi wa Civitas Maxima, shirika lisilo la kiserikali kutoka Uswisi linalowakilisha waathirika hao.

Adhabu hii ni ya kipekee kwa Liberia, ambapo viongozi wengi waliohusika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe bado wanashikilia nafasi muhimu za kiuchumi na kisiasa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.