Pata taarifa kuu
DRC-MONUSCO-USALAMA

Askari wawili wa MONUSCO watoweka DRC

Askari wa Monusco wametakiwa kufanya kilio chini ya uwezo wao kuhakikisha wenzao wawili wanapatikana," Msemaji wa MONUSCO, Florence Marchal amesema.
Askari wa Monusco wametakiwa kufanya kilio chini ya uwezo wao kuhakikisha wenzao wawili wanapatikana," Msemaji wa MONUSCO, Florence Marchal amesema. ©MONUSCO

Askari wawili wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) hawajulikani walipo, siku nne baada ya shambulio la msafara wao, shambulio lililoendeshwa na wanamgambo kusini-mashariki mwa nchi hiyo, msemaji wa Monusco ameliambia shirika la habari la AFP Jumanne wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

"Msafara wa magari ya kikosi cha askari wa Umoja wa Mataifa uliwashambuliwa siku ya Ijumaa wiki iliypita na waasi wa Ma Mai Mai katika jimbo la Tanganyika, tangu wakati huo askari wawili wa kikosi hicho kutoka Benin hawajulikani walipo," msemaji wa MONUSCO, Florence Marchal, amesema.

"Askari wa Monusco wametakiwa kufanya kilio chini ya uwezo wao kuhakikisha wawili hao wanapatikana," Bi Marchal ameongeza.

Msafara ulioshambuliwa ulikua wa "magari mawili, na askari 13", "wengine 11 wako salama kabisa," amesema Bi Marchal, akihohojiwa na shirika la habari la AFP.

Mnamo mwezi Desemba, walinda amani kumi na tano kutoka Tanzania waliuawa baada ya ngome yao kushambuliwa na waasi wa Uganda wa Allied Democratic Forces (ADF) katika tarafa ya Beni kaskazini-mashariki mwa DRC.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.