Pata taarifa kuu
MAURITANIA-SENEGAL-WAHAMIAJI

Mauritania: Wahamiaji kutoka Senegal warudishwa nyumbani

Ghorofa ya kwanza ya kituo cha Thiès, ambako kundi la kwanza la wahamiaji kutoka Senegal walirejeshwa nymbani kutoka Mauritania.
Ghorofa ya kwanza ya kituo cha Thiès, ambako kundi la kwanza la wahamiaji kutoka Senegal walirejeshwa nymbani kutoka Mauritania. © Vladimir Cagnolari

Serikali ya Mauritania imeamuru kufukuzwa kwa wahamiaji 53 wa Senegal waliokamatwa siku za hivi karibuni katika mji wa Nouadhibou walipokua wakijaribu kufikia kuingia Visiwa vya Kanari nchini Hispania kwa kutumia mtumbwi.

Matangazo ya kibiashara

Wahamiaji hao waliondoka katika mji wa Senegal wa Thiès, Jumatatu, Mei 28, wakitumia meli wakijaribu kuelekea Visiwa vya Kanari kabla ya boti lao kupata tatizo la kiufundi karibu na pwani ya Mauritania ya Nouadhibou. Nahodha wa boti hilo alikimbia na abiria walirudishwa nyuma na manuari ya kijeshi ya Mauritania kabla ya kuhamishiwa Nouadhibou na kusafirishwa Nouakchott.

Viongozi wameamua kuwarudisha nyumbani baada ya kuwasili katika mji wa Nouakchott. Kundi la kwanza la wahamiaji hao wameondoka nchini Mauritakia kuelekea nchini Senegal, kwa mujibu wa kiongozi wa shirika la raia wa Senegal waishio nchini Mauritania. "Siku ya Jumatatu, kundi la kwanza la wahamiaji 21 waliondoka kuelekea Senegal, Assane Gueye ameiambia RFI. Wengine watafuata hivi karibuni. Niliweza kuwaona, niliona jinsi walivyokaribishwa, katika mazingira mazuri tu".

Assane Gueye ndiye anayewasiliana moja kwa moja na raia hao wenzake. Amesema ameshangaa kuona idadi kubwa ya raia wa Senegal katika boti moja. "Kabla ya hapo, ulikua ukikuta raia kutoka nchi mbalimbali katika boti moja, hasa watu kutoka Gambia, Guinea na Mali. Lakini kwa sasa, kulikuwa na raia 53 kutoka Senegal, kwa kweli nashangaa. Raia wengine 32 waliyobaki katika kituo cha Nouakchott watasafirishwa kurudi nyumbani katika siku zijazo baada ya kusainiwa sheria ya kuwafukuza nchini.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.