Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mali yakiri kuhusika kwa askari wake katika mauaji ya halaiki

Askari wa Mali wakipiga doria katika mji wa Menaka wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Mei 9, 2018.
Askari wa Mali wakipiga doria katika mji wa Menaka wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Mei 9, 2018. Sebastien RIEUSSEC / AFP

Serikali ya Mali imekiri kuwa baadhi ya askari wake walihusika katika "ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu uliosababisha vifo vya watu wengi". Kauli hii inakuja siku chache baada ya makaburi ya halaiki kugunduliwa katikati mwa nchi. Serikali ya Mali imesema iko tayari "kukubali" makosa hayo.

Matangazo ya kibiashara

Miili ya watu 25 ilipatikana katika siku za hivi karibuni katika mkoa wa Mopti (katikati mwa nchi), wikimoja baada ya mfululizo wa operesheni ya kamatakamata iliyoendeshwa na jeshi la Mali.

"Ujumbe wa uangalizi uliotumwa katika eneo hilo umethibitisha kuwepo kwa makaburi ya halaiki na hivyo kuhusisha baadhi ya askari wa Mali (Fama) katika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu uliosababisha vifovya watu wengi huko Nantaka na Kobaka, katika mkoa wa Mopti," amesema Waziri wa Ulinzi, Tiéna Coulibaly, akinukuliwa katika taarifa ya serikali.

"Waziri ameagiza mwendesha mashitaka wa mahakama ya kijeshi kuanzisha uchunguzi. Amesema yuko tayari kupambana dhidi ya ukatili na kutoa wito kwa jeshi la Mali (Fama) kuheshimu mikataba kuhusu haki za binadamu na sheria ya kimataifa ya kibinadamu katika uendeshaji wa operesheni za kijeshi, "nakala hiyo imeongeza.

"Saa chache zilizopita, tulitahadharishwa na Waziri wa Ulinzi mara moja alitumwa tume ya waangalizi. Matokeo ya uchunguzi huo yatazingatiwa kwa umakini," alisema Jumanne jioni Rais Mali, Ibrahim Boubacar Keïta, alipokua akiwapokea wanaharakati wa haki za binadamu mjini Bamako.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.