Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Magaidi kumi na tano wauawa Mali

Askari wa Ufaransa kutoka kikosi cha Barkhane huko Timbamogoye, Mali, Machi 10, 2016.
Askari wa Ufaransa kutoka kikosi cha Barkhane huko Timbamogoye, Mali, Machi 10, 2016. © AFP

Kikosi cha askari wa Ufaransa nchini Mali (Barkhane) kimetangaza kwamba kwa ushirikiano na jeshi la Mali wamefaulu kuvunja kundi moja la wapiganaji wa kijihadi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji zaidi ya kumi na tano wa kijihadi waliangamizwa tarehe 22 Juni katika mapigano na askari wa Mali na wale wa kikosi cha Barkhane kaskazini mwa Mali,uongozi wa majeshi ya Ufaransa umebaini.

Katika taarifa yake, uongozi wa majeshi ya Ufaransa unabaini kwamba "kikosi maalumu cha makomando wa Mali wanaoshiriki katika kikosi cha askari wa Ufaransa nchini humo Barkhani kilipambana na magaidi ishirini katika eneo la msitu wa eneo la Inabelbel" kaskazini Magharibi mwa Timbuktu.

"katika mapigano hayo magaidi zaidi ya kumi na tano waliuawa na wengine walikamatwa, huku silaha zao nyingi zikiharibiwa vibaya, " uongozi wa Majeshi ya Ufaransa umesema.

Operesheni ya pamoja kati ya jeshi la Mali na askari wa wa kikosi cha Barkhane "zimekua zikisambaratisha makundi ya kigaidi katika maeneo yao maficho na kupelekea kupatikana kwa matokeo mazuri," umeongeza.

Tangu mwaka 2013, makundi ya kijihadi ambayo yamekua yakitishia mji mkuu wa Mali, Bamako, yamesambaratishwa na kwa kiasi kikubwa yalitimuliwa kaskazini mwa Mali, lakini jeshi la Mali, kikosi cha Ufarans Barkhane na kikosi cha Umoja wa Mataifa (Minusma) lwameshindwa mpaka sasa kuyaweka chini ya himaya yao maeneo yanayosalia.

Tangu mwa 2015, mashambulizi haya yameenea katikati na kusini mwa Mali na hali hii imeenea kwa nchi jirani, hasa Burkina Faso na Niger.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.