Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-ERITREA-USHIRIKIANO

Rais wa Eritrea kukutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (kushoto) na Rais wa Eritrea Issayas Afewerki (kulia).
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (kushoto) na Rais wa Eritrea Issayas Afewerki (kulia). © ASHRAF SHAZLY, Sumy SADRUNI / AFP

Tangu Jumanne wiki hii, ujumbe unaojumuisha Waziri wa Mambo ya Nje Osman Saleh na Mshauri wa rais wa Eritrea Yemane Gebreab ulikua nchini Ethiopia kwa minajili ya kuanza kwa mazungumzo ya kwanza tangu miaka 20 iliyopita kati ya nchi hizi mbili jirani za Pembe ya Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Eritrea, ziara ya ujumbe wa Eritrea nchini Ethiopia imetamatika.

Baada ya miaka mingi ya mvutano, vita kati ya mwaka 1998 na 2000 na mgogoro wa mpaka unaoendelea, mazungumzo haya ya kwanza yanayolenga kukomesha moja kwa moja mgogoro ni ya kihistoria. Kwa mujibu wa vyanzo kutoka serikali za nchi hizi mbili Rais wa Eritrea amepanga kukutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia.

Issayas Afewerki, Rais wa Eritrea, na Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia watakutana "hivi karibuni". Kulingana na kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia akinukuliwa na vyombo vya habari nchini humo amesema "ziara ya ujumbe wa Eritrea imeweka mambo sawa kwa kurejesha amani kati ya nchi hizo mbili".

Kuanzishwa kwa mahusiano kati ya nchi hizi mbili haukufikiriwa wiki chache zilizopita, wakati ambapo mvutano kuhusu mipaka ulikua ukiendelea. Hata hivyo, Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia, Abiy Ahmed, alitangaza mwanzoni mwa mwezi Juni nia yake ya kuleta amani kati ya nchi hizi mbili. Na kutekeleza makubaliano ya mwaka 2002 ambayo yanaeleza mpaka mpya kama ishara ya kuiridhisha Eritrea.

Mabadiliko makubwa ya kisiasa na ishara "chanya" kwa Rais wa Eritrea Issayas Afewerki, ambaye alitangaza siku chache baadaye ziara ya ujumbe huu wa serikali.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.