Pata taarifa kuu
SIASA-MALAWI-PETER MUTHARIKA

Chama tawala nchini Malawi chakutana kumchagua naibu kiongozi

Rasia wa Malawi ambaye pia ni kiongozi wa Chama tawala cha DPP, Profesa Peter Mutharika
Rasia wa Malawi ambaye pia ni kiongozi wa Chama tawala cha DPP, Profesa Peter Mutharika The Maravi Post

Chama tawala nchini Malawi cha Democratic Progressive Party (DPP) kinafanya mkutano wake hivi leo ambao utamchagua Naibu Kiongozi kuchukua nafasi ya Saulos Chilima ambaye alitangaza kung'atuka mwezi uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi atakayechaguliwa huenda akawa mgombea mwenza wa rais Peter Mutharika katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Mei, mwakani.

Wakati wajumbe wa mkutano huo wakikutana Mjini Blantyre, gazeti la Nyasa Times limearifu katika toleo lake la leo kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo Dr. George Chaponda alianguka kabla ya kuhutubia wajumbe wa mkutano wa uchaguzi.

Wagombea wengine wa nafasi ya naibu rais ni Henry Mussa na Joseph Mwanamveka.

Chini ya mwaka mmoja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi kumeripotiwa migawanyiko ndani ya chama tawala inayotajwa kusababishwa na makundi yanayojipanga kuwania uongozi katika uchaguzi ujao.

Ripoti ya Mwandishi wa RFI Kiswahili, Fredrick Nwaka

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.