Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-ERITREA-USHIRIKIANO

Eritrea na Ethiopia zafufua uhusiano wa kidiplomasia

Picha ya kumbukumbua) Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, hapa Aprili 11, 2018 katika mkoa wa Oromia.
Picha ya kumbukumbua) Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, hapa Aprili 11, 2018 katika mkoa wa Oromia. REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya majirani wawili, Ethiopia na Eritrea ulivunjika miaka 20 iliyopita. Hatimaye nchi hii mbili zilizokua katika uhasama zimefufua uhusiano wao wa kidiplomasia, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alitangaza siku ya Jumapili (Julai 8) huko Asmara, baada ya kupokelewa kwa hesima kubwa na rais wa Eritrea Issayas Afewerki.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya mazungumzo na rais wa Eritrea, Waziri Mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiy alitangaza kufungua upya balozi za nchi hizo mbili katika miji yao mikuu, na pia kufungua upya mipaka inayotenganisha nchi hizo mbili.

"Tumekubaliana kuwa zafari za ndege kutoka na kwenda nchi zetu mbili zitaanza hivi karibuni, na pia bandari zetu zifunguliwe kwa meli kutoka nchi zetu mbili, ili watu waweze kuingia na kutoka kati ya nchi hizo mbili na balozi zetu zifunguliwe," Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema.

Mapema kwenye Twitter, afisa mwandamizi kwenye ofisi ya waziri mkuu wa Ethiopia alitangaza kuwa mawasiliano ya simu ya moja kwa moja yamerejeshwa kati ya Eritrea na Ethiopia.

Kwa siku nzima, picha ya umati wa watu wakishangilia katika mitaa ya Asmara na mapokezi ya shangwe ya rais Isaias Afewerki wa Eritrea kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiy alipokua akishuka ndege yamekua yakirushwa kwenye runinga ya taifa ya Eritrea.

Hatua ya kuelekea amani

Mwezi mmoja uliopita, waziri mkuu mpya wa Ethiopia aliwashangaza wengi kwa kutangaza nia yake ya kutekeleza makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka wa 2000 na Eritrea ambayo yanaeleza kurejeshwa kwa maeneo yaliyopokonywa kwa nchi hiyo.

Eritrea inaendelea kukumbwa na hali mbaya ya kisiasa na kiuchumi. Utawala nchini humo unakabiliwa na vikwazo vya kijeshi. Wadadisi wanasema vyote hivyo huenda ni miongoni mwa vikwazo vilivyomshawishi Issayas Afewerki.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.